Kuhusu PLF Hub
Precision Livestock Hub (PLF Hub) inalenga kuleta mapinduzi katika ufugaji bora kupitia teknolojia za kisasa na mbinu bunifu.

Kituo hiki kilianzishwa kama sehemu ya mpango wa utafiti unaolenga kutathmini ufanisi wa teknolojia za kisasa za ufugaji barani Afrika. Mpango huu umeundwa ili kuimarisha matumizi ya teknolojia bunifu katika ufugaji wa mifugo, lengo kuu likiwa ni kuongeza uzalishaji, ufanisi, na faida kwa wafugaji. Kwa kushirikiana na taasisi za utafiti na wadau wa sekta, tunalenga kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya ufugaji.

Kituo chetu kitakuwa mahali ambapo teknolojia mbalimbali zinajaribiwa. Kwa sasa kituo hiki kitakuwa kikijaribu teknologia ya smaXtec bolus. Wakati tafiti nyingine zikiendelea kufanyika katika mashamba ya wafugaji madogo na makubwa nchini Tanzania, PLF Hub itafanya majaribio mbalimbali ili kupima ufanisi wa teknolojia hii katika mazingira yaliyodhibitiwa. Hii itatuwezesha kutoa mapendekezo sahihi kwa wafugaji kuhusu matumizi bora ya teknolojia hii.

Subscribe
to our newsletter
Miundombinu iliyopo

Pia  moja ya vitu PLF Hub inalenga kufanya ni kujenga banda la kisasa la ng’ombe ambalo litakuwa mfano bora wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa. Eneo hili litaonyesha mbinu bora za ujenzi wa mabanda, likizingatia vitu muhimu, kama vile ukubwa wa banda, sehemu za chakula na kupumzikia ng’ombe,n.k. Wafugaji watapata fursa ya kutembelea na kujifunza kutoka kwetu, wakipata maarifa kuhusu mbinu  za kujenga banda bora na usimamizi wa mifugo.

Pamoja na banda la mifugo, tunaanzisha mashamba maalum kwa ajili ya kulima malisho yanayofaa hali ya hewa mbalimbali na yenye lishe bora kwa wanyama. Mashamba haya yataonyesha kilimo cha mazao mbalimbali ya malisho yanayofaa kwa hali ya hewa ya eneo husika, yakitoa maarifa ya vitendo kwa wafugaji kuhusu uzalishaji wa chakula cha mifugo chenye ubora wa hali ya juu. Kwa kuunganisha uzalishaji wa malisho na mbinu za kisasa za ufugaji, tunalenga kutoa mazingira ya kujifunza yanayowezesha wafugaji kuboresha usimamizi wa mifugo yao na uzalishaji wa shamba kwa ujumla.

Jiunge nasi
Shirikiana na PLF Hub: Kuendeleza Ufugaji Bora na wa kisasa
PrecisionLF

Katika PLF Hub, tumejizatiti kuleta mapinduzi katika ufugaji wa maziwa kwa kuunganisha teknolojia za kisasa na mbinu bunifu. Dhamira yetu ni kuongeza tija, uendelevu, na faida kwa wafugaji kupitia utoaji wa mafunzo maalum na rasilimali muhimu.Tunatambua umuhimu wa ushirikiano katika kufikia malengo yetu. Tunakaribisha mashirika na watu binafsi kushirikiana na PLF Hub kkuendeleza kile tulichokianzisha.

Ushiriki wako unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya juhudi zetu na kuleta tija katika jamii yetu . Tuko tayari kujadili kwa pamoja namna tutakavyo shirikiana na malengo yetu ya pamoja.

Asante kwa kuzingatia fursa hii ya kufanya kazi pamoja kuelekea mustakabali endelevu na wenye mafanikioo.Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia plfhub@nm-aist.ac.tz./+255763973003

Guidebook
Apply for Admission or some other Call to Action