Mradi huu unalenga kufanya tathmini ya ufanisi wa teknolojia za kisasa za ufugaji barani Afrika. Mradi huu wa utafiti ni wa miaka mitatu (2023-2025) na unafadhiliwa na Bill & Melinda Gates Foundation. Mradi huu unalenga kutatua changamoto za ufugaji pamoja na kufanya tathimini ya matumizi ya teknolojia za kisasa za ufugaji wa mifugo barani Afrika. Lengo ni kuwasaidia wafugaji wa ng’ombe wa maziwa na wa nyama kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kama vile; magojwa ya mifugo, ukosefu wa taarifa na kushindwa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati juu ya mifugo yao, hali inayochangia kushuka kwa uzalishaji.
Kupitia njia za utafiti na hatua mbalimbali zitakazochukuliwa katika mradi huu; lengo letu ni kuwajengea wafugaji uwezo na kuweka miundombinu itakayoweka misingi ya kuanzishwa kwa matumizi ya teknolojia kwa wafugaji pamoja na teknolojia nyingine zenye makusudio hayo. Hii itachangia katika kuongeza uzalishaji endelevu kwa wafugaji wadogo wa ngombe wa maziwa nchini Tanzania na maeneo mengine kusini mwa Jangwa la Sahara. Ili kufikia lengo hili, mradi unategemea kutekeleza shughuli za utafiti kama ifuatavyo.