Tumejipanga kusambaza bolas za smaXtec katika vijiji vitano ndani ya Wilaya ya Hai—Kilanya, Nronga, Mroma, Lukani, na Foo.
Mradi huu wa kipekee unalenga kuboresha afya ya mifugo na kuongeza uzalishaji wa maziwa kupitia teknolojia ya kisasa ya smaXtec bolus.
SmaXtec bolus Bolasi ni kifaa cha kisasa kinachowekwa ndani ya tumbo la ng’ombe, ambapo hufuatilia kwa mfululizo viashiria muhimu vya afya kama vile joto la mwili, ulaji wa ng’ombe, unywaji wa maji, na kutoa taarifa mbalimbali kama ng’ombe anapata chakula/maji ya kutosha, anakaribia kuingia joto, au anadalili za ugonjwa n.k. Bolas hii inamsaidia mfugaji kugundua mapema matatizo ya kiafya ya ng’ombe wake, kuboresha mafanikio ya uzazi, na kuhakikisha mikakati bora ya kulisha..
Endelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya huu mradi na jinsi mradi huu unavyolenga kuleta chachu ya maendeleo katika sekta ya kilimo na ufugaji .
Kwa kutumia teknolojia hii, wafugaji watawezeshwa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi yanayoboresha ustawi na kuongeza uzalishaji.