Uwekaji wa Boluses kwa ngombe wa maziwa katika wilaya ya Hai

Tumejipanga kusambaza bolas za smaXtec katika vijiji vitano ndani ya Wilaya ya Hai—Kilanya, Nronga, Mroma, Lukani, na Foo. 

Mradi huu wa kipekee unalenga kuboresha afya ya mifugo na kuongeza uzalishaji wa maziwa kupitia teknolojia ya kisasa ya smaXtec bolus.

SmaXtec bolus Bolasi  ni kifaa cha kisasa kinachowekwa ndani ya tumbo la ng’ombe, ambapo hufuatilia kwa mfululizo viashiria muhimu vya afya kama vile joto la mwili, ulaji wa ng’ombe, unywaji wa maji, na kutoa taarifa mbalimbali kama ng’ombe  anapata chakula/maji ya kutosha, anakaribia kuingia joto, au anadalili za ugonjwa n.k. Bolas hii inamsaidia mfugaji kugundua mapema matatizo ya kiafya ya ng’ombe wake, kuboresha mafanikio ya uzazi, na kuhakikisha mikakati bora ya kulisha..

placeholder

 Endelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya huu mradi na jinsi mradi huu unavyolenga kuleta chachu ya maendeleo katika  sekta ya kilimo na ufugaji .


Kwa kutumia teknolojia hii, wafugaji watawezeshwa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi yanayoboresha ustawi na kuongeza uzalishaji.

Tags

Join event

2024-10-12 8:00 am 2024-11-12 8:00 pm UTC-3 Uwekaji wa Boluses kwa ngombe wa maziwa katika wilaya ya Hai The PLF project would like to invite you to their events. Hai District , Arusha
Add to Calendar
You already has been joined the event.
×
Thank you! You joined the event.
×